Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa
Japan umethibitisha kwamba kukaa kwa mda mrefu na kutazama vipindi vya
televisheni kwa masaa mengi kunahatarisha afya kwani huhusishwa na
maradhi yanasababisha mzunguko wa damu mwilini kutokuwa sawa.
Watafiti
hao wanasema, hali hiyo pia huenda ikasababisha damu kuganda na
kutengeneza vidonge katika sehemu kama vile miguu, na iwapo mgando huo
utasukumwa na nguvu za mzunguko wa damu na kuingia sehemu kama vile
mapafu, husababisha vifo.Utafiti huo ulihusiha watu zaidi ya 86,000 ambao hupendelea kutazama televisheni katika mida mbalimbali kwa siku.
Kisha afya zao zilifuatiliwa kwa zaidi ya miaka 19 tangu mwaka 1988 hadi 1990.
Matokeo yalikuwa kila muda wa masaa mawili yalipopita mtu akikaa kutazama televisheni, nayo hatari ya kupata ugonjwa huo wa mapafu uitwao ‘Fatal pulmonary embolism’ ulioongezeka kwa asilimia 40%.
Iligundulika pia kuwa waliotazama vipindi vya televisheni kwa zaidi ya saa 5 walikuwa katika hatari zaidi kuliko waliotazama televisheni kwa mda wa chini ya saa 3.
Zaidi ya hayo watu huambatanisha kitendo cha kukaa na kutazama televisheni huku wakila vitafunio kama vile Popcorns na Crisps ambavyo pia huwasababishia si tu mwili kukosa mazoezi bali pia kuongezeka kwa uzito unaohatarisha afya.
Post A Comment:
0 comments: