KONGAMANO LA MSAADA KWA DARFUR,QATAR

Share it:

Hali ya njaa katika Darfur
Taifa la kiarabu la Qatar ndio mwenyeji wa mkutano wa siku mbili kuhusu maendeleo na ukarabati katika jimbo la Darfur nchini Sudan.
Kabla ya mkutano huo kufunguliwa rasmi, Uingereza ilitangaza kuwa itatoa kima cha pauni milioni 33.Kongamano hilo linalenga kuchangisha dola bilioni 7.2 kama msaada wa maendeleo unaonuia kulifanya Darfur eneo la kujitegemea.
Takriban watu 300,000 wanaaminika kufariki wakati wa mapigano ya mwongo mmoja katika jimbo hilo, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.
Share it:

Post A Comment:

0 comments: