Waafrika wanaoishi ndani na nje ya mji mkubwa zaidi
wa kibiashara nchini India, Mumbai (Bombay), wanalalamika
kuhusu ubaguzi wa rangi na polisi kuwanyanyasa kila mara.
Sambo Davis ni raia wa Nigeria ambaye amemuoa mwanamke wa kihindi na wanaishi naye mjini Mumbai.Stakabadhi zake zote ni halali lakini alikamatwa na polisi hivi karibuni baada ya kushukiwa kuhusika na bishara za mihadarati.
Yeye pamoja na waafrika wengine 30, walizuiliwa kwa masaa mengi kabla ya kuachiliwa na kuombwa msamaha.
Lakini siku iliyofuata, bwana Davis alisema kuwa alishtushwa sana kusoma kwenye magazeti kuwa walikuwa wamekematwa kwa kuhusika na biashara haramu ya mihadarati.
Post A Comment:
0 comments: