NYOTA wa vichekesho nchini Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’
ambaye wiki iliyopita alitawala kwenye vyombo mbalimbali vya habari
baada ya kuvuta jiko, mtoto mrembo Monica, amesema kati ya vitu ambavyo
hawezi kuvisahau maishani mwake ni pamoja na adhabu ya kufinywa
aliyokuwa akipewa na mama yake.
Akizungumza na Juma3tata, Masanja alisema kuwa nidhamu aliyonayo hivi
sasa imetokana na malezi aliyopewa na marehemu mama yake alipokuwa
anamuonya pale alipofanya makosa mbalimbali.
“Utoto una mambo mengi, niseme ukweli kuwa mimi nilikuwa mtundu mno.
Lakini mama yangu hakutaka niharibike, alikuwa akiniadhibu kila
ninapofanya makosa na mara nyingi alikuwa akinifinya.
“Mama yangu ndiye amenifanya niwe na nidhamu mpaka sasa kwa sababu
kipindi kile nakumbuka niliwahi kufinywa hadi mbele za wageni na
kutakiwa kuonyesha tabasamu.
“Nilifinywa kwa makosa tofauti tofauti, si unajua tena tabia za
kitoto, fujo za hapa na pale ndiyo vile mama anapitisha mkono chini ya
meza na kunifinya halafu ananikazia jicho ili usilie,” anasema Masanja
na kuongeza:
“Lakini mimi najivunia kwa hilo, wala simlaumu mama yangu, maana
alininyoosha na kunitengenezea maisha ya nidhamu hadi utu uzima huu
unaoniona nikiwa tayari nimeshaingia kwenye ndoa yangu. Nidhamu
niliyonayo, sifa ziende kwa mama yangu.”
Navigation
Post A Comment:
0 comments: