Zaidi ya watu 2,000 mashuhuri duniani wametoa heshima zao za mwisho kwa hayati Margaret Thatcher katika mkusanyiko mkubwa wa watu tangu mazishi ya mamake malkia wa Uingereza mwaka 2002.
Jeneza la Bi Thatcher, lilibebwa na kupitishwa katika barabara za London likisindikizwa na waombolezaji pamoja na vikosi vitatu vya jeshi la taifa.
Waziri mkuu David Cameron amesma kuwa heshima hizo zilistahili kwa mtu mashuhuri kama Thatcher.
Polisi elfu nne wamshika doria mjini London , mji ambao umejionea idadi kubwa ya watu waliojitokeza kushuhudia mazishi hayo.
Kulikuwa na taarifa za maandamano dhidi ya Thatcher ingawa sio makubwa kama ilivyotarajiwa.
Mkusanyiko wa watu katikakanisa la Mtakatifu Paul ulijuimsha familia ya Thatcher pamoja na waziri wakuu wa zamani ikisemo Tony Blair, Gordon Brown na Sir John Major, mawaziri wa sasa na wale waliohudumu kama serikali ya Bi Thatcher.
Majonzi yalishuhudiwa pamoja na kicheko mara kwa mara huku Askofu wa London, Richard Chartres akiwakumbusha watu kuhusu Thatcher na kimsifu kwa ukakamavu wake.
Thatcher alikuwa na ushawishi na mwenye utata na lifariki wiki jana baada ya kuugua kiharusi
Maelfu ya watu na maafisa wa kijeshi walipiga foleni katika barabara kuu za mjini London kuusindikiza mwili wake Bii hatcher.
Post A Comment:
0 comments: