Madonda ya tumbo ni nini?
Haya ni madonda yanayoshambulia tumbo la chakula{stomach} na utumbo mdogo {douedunum}.
chanzo ni nini?
Sababu kuu mbili muhimu zimegundulika ndio chanzo kikuu cha madonda ya tumbo kwa binadamu nazo ni.
Helocobactor Pylori: hawa ni bacteria ambao ni chanzo kikubwa cha ugonjwa huu na asilimia kubwa ya wagonjwa wamekutwa na bacteria hao wanapoenda kupimwa.
Non steroidal antiflamatory drugs: hichi ni kikundi cha dawa za maumivu ambazo kitaalamu zinafanya kazi kwa kuondoa hormone iitwayo kitaalamu kama prostiglandins ambayo ni muhimu kwa kutunza tumbo lisipate madhara. mfano diclofenac, ibuprofen, peroxicam, meloxicam na etc
Sababu zingine ni:
Uvutaji wa sigara: utafiti umeonyesha asilimia kubwa ya watu waliokutwa na ugonjwa huu walijuhusisha na uvutaji wa sigara lakini haifahamiki ni jinsi gani sigara inaleta mdonda haya.
Mgandamizo wa mawazo: mtu anapokua na mawazo sana{stress}, mwili hutengeneza hormone inayoitwa kitaalamu kama adrenaline ambayo hukunja mishipa mikubwa na midogo ya damu{vasoconstriction of arteries and arterioles} ya mwili mzima.
Mishipa hiyo ambayo na tumboni ipo, inapojikunja husababisha vidonda{ulcer}.
Kwasababu ya kukosekana damu ya kutosha kwenye seli za tumboni.
Genetics: baadhi ya koo zimeonyesha kurithi ugonjwa huu na japokua haijathibitika mahusiano yake yakoje.
Dalili za madonda yalioko tumboni.{gastric ulcers}
Kichefuchefu na kupungua uzito kwani aina hii ya madonda ya tumbo humfanya mtu aogope chakula.
Maumivu makali wakati wa kula kwasababu chakula huingia tumboni na kuanzisha maumivu hapo hapo.
Kujisaidia choo nyeusi ni dalili kwamba madonda yanavuja damu.{digested blood is always black} dalili za madonda ya kwenye utumbo mdogo.
Maumivu makali masaa matatu mapaka manne baada ya kula.
Kuongezeka uzito kwani maumivu ya aina hii ya madonda humfanya mtu ale sana ili kupata nafuu.
Kutoa choo nyeusi.
Vipimo vya kugundua madonda ya tumbo hospitalini:Bariaum meal na barium swallow:
Hichi ni kipimo ambacho mgonjwa anapewa aina flani ya kimiminika na kunywa kisha picha ya x ray hupigwa kufuatisha kile kimiminika kuangalia kama kuna sehemu ina shape ambayo si ya kawaida tumboni.
Esophagogastroduodenoscopy:
hichi ni kipimo ambacho aina flani ya mpira ambao una camera kwa mbele, hupitishwa mpaka tumboni na kuonyesha picha ya tumbo kwenye screen kuangalia kama kuna tatizo lolote.
Ultrasound scan:
Kipimo hichi hutumia mashine ambayo mgonjwa hutakiwa kunywa maji ili sehemu ya tumbo na utumbo zipate kuonekana vizuri wakati wa kupima.
Nb: vipimo hivi havipatikani kirahisi nchini kwetu hivyo madaktari hutumia akili zao ambazo zimefundishwa kutambua ugonjwa huo bila ata vipimo.
MATIBABU;
Ugonjwa huu unatibika na kupona kabisa sio kama watu wengi wanavyodai hauponi na kukaa nao miaka huku wakiteseka.
Mchanganyiko wa dawa kitaalamu kama triple therapy umeonyesha kutibu ugonjwa huu kabisa .{omeprazole, amoxycline,metronidazole} au {lansoprazole, scenidazole, clarithromycin}
Pia unaweza kutumia mchanganyiko wa cimetidine, amoxyline na metronidazole kulingana na uwezo wa kuzipata dawa hizo
Dawa za kupunguza tindikali tumboni ni nzuri sana kupunguza dalili na maumivu. Mfano magnesium transilicate tablets.
Kwanini watu wengi hawaponi ugonjwa huu?
dozi ya ugonjwa huu sio chini ya wiki nne, lakini utakuta mtu anameza dawa kwa wiki moja tu na kuacha au pale anaposikia maumivu tu ndo anameza.
kuendelea kunywa pombe na kuvuta sigara wakati ugonjwa bado haujapona.
Kula vyakula vya moto sana au baridi sana kipindi cha ugonjwa.
Kula nyama kwa wingi kipindi cha matibabu.{ nyama inapoliwa tindikali nyingi hutolewa na nyongo kumeng”enya nyama hiyo{ lakini pia tindikali hiyo ni hatari sana kwa vidonda vya tumbo}
Matibabu ya asili:
Utafiti wa chuo kikuu cha stanford umebaini unywaji wa juice ya kabechi mbichi kwa kiwango cha 250mils{ujazo wa kikombe cha chai} kila baada ya masaa sita umeonyesha kutibu kabisa tatizo hili ndani ya wiki mbili tu.
MWISHO;
Post A Comment:
0 comments: